LISHE
YA KUKU:
Ili kuku waweze kuishi, kukua vizuri, kunenepa na kutaga mayai mengi ni
lazima wale chakula kingi na chenye ubora unaotakiwa. Uwingi na ubora wa lishe ya kuku unaweza
kuainishwa katika makundi ya vyakula kama ifuatavyo:
1. Vyakula vya kutia nguvu
2. Vyakula vya kujenga mwili
3.
Vyakula vya kuimarisha mifupa
4.
Vyakula vya kulinda mwili
5.
Maji.
Makundi ya vyakula:
- Vyakula vya kutia nguvu:
Vyakula
vya mifugo vifuatavyo vinawekwa katika kundi hili;
a. Pumba za mahindi, pumba laini za mpunga, na, pumba laini za ngano.
b. Nafaka kama vile mtama , chenga za mahindi ,chenga za mchele, uwele , na
ulezi
c. Mimea ya mizizi kama vile muhogo, viazi vitamu na magimbi. Kabla ya
kulisha kuku hakikisha mizizi hiyo inalowekwa kwa muda wa saa moja au kupikwa
kabla ya kukausha ili kuondoa sumu ambayo kwa asili imo katika vyakula vya aina
hii.Inashauriwa kuwa mizizi hiyo ilishwe
kwa kiasi cha asilimia 10% ya chakula chote anacholishwa kuku.
Katika kundi hili la kutia nguvu
,vyakula vya mafuta kama vile mafuta ya kutoka kwenye vyakula vya mafuta kama
mashudu ya mimea ya mafuta, mafuta ya samaki husaidia kuongeza nguvu na joto
mwilini. Vyakula vya kutia nishati huchangia asilimia 60-70 ya mchanganyiko
wote wa chakula.
1.
Vyakula vya kujenga mwili:
Ø Mashudu :Haya ni makapi ya mbegu za mimea aina ya mikunde na vyakula v
vinavyotoa mafuta kama vile alizeti, mawese, karanga, soya ,korosho, na ufuta .
Ø Damu ya wanyama iliyokaushwa (waliochinjwa na kukaguliwa), hii inafanywa
ili kuepusha uwezekano wa kuku kupata magonjwa ya kuambukiza .
Ø Mabaki ya samaki ya samaki/dagaa na nyama.
Ø Vyakula asilia kama vile minyoo, mayai ya mchwa, Masalia ya nyama toka
kwenye ngozi/mifupa, wadudu walioteshwa kutokana na damu au nyama iliyooza na
vyakula vya aina nyingine.
Ø Vyakula hivi huchangia asilimia 20 hadi 30% ya mchanganyiko wote wa
chakula cha kuku.
2. Vyakula
vya kuimarisha mifupa(madini): a)Hivi ni vyakula vya madini ambavyo
huhitajika kwa ajili ya kujenga mifupa, maganda ya mayai, kukua na kuuweka
mwili wa ndege (kuku) katika hali ya afya njema kwa ujumla.
b) Madini ya muhimu ni madini ya chokaa (calcium) na fosiforasi (phosphorus).
Ili kuku watage mayai yenye ganda gumu ni lazima wapate madini ya chokaa
maganda ya konokono na mayai yaliyosagwa vizuri. Lakini inapendekezwa kwamba
unapoongeza madini ya fosforasi inakubidi uongeze pia madini ya chokaa kadri
inavyopasa ,kwasababu kiwango cha aina moja kikizidi kuliko cha aina nyingine
husababisha upungufu wa kile kidogo
Viinilishe
vya madini vinavyotakiwa ni pamoja na;
Ø Majivu ya mifupa yaliyosagwa vizuri, unga uliosagwa wa magamba ya konokono
wa baharini, konokono wa nchi kavu na maganda ya mayai yaliyochomwa . Kabla
maganda ya mayai na nyumba za konokono havijatumika inashauriwa yachomwe moto
mkali au yachemshwe ili kuua vijidudu vya maradhi.
Ø Chumvi ya jikoni
Ø Madini
yaliyotengenezwa viwandani kama vile Di-calcium phosphate
Ø Magadi (kilambo).
4. Vyakula
vya kulinda mwili:
Kundi hili linajumuisha vyakula vya mbogamboga kama
vile;
Ø Mchicha, samadi ya ng’ombe ambayo haijakaa muda mrefu baada ya kunyewa,
mchicha pori, Chinese kabeji n.k.
Ø na Mchanganyiko wa vitamini uliotengenezwa na viwanda vya madawa
(vitamin premix).
Ø Jua ni muhimu katika kuhakikisha vitamini A na D zinatumika vizuri
mwilini, kwahiyo banda ni lazima lijengwe kwa mtindo ambao unaruhusu mwanga
kupita hasa nyakati za asubuhi na jioni.
Ø Chakula cha kuku wanaofugwa ndani ni lazima kichanganywe na vitamini
zinazotayarishwa viwandani.
KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU:
Njia za kuchanganya chakula cha kuku;
Kuna
njia kuu mbili za kuchanganya chakula cha kuku, nazo ni;
Ø Kuchanganya chakula kwa mashine;
o Njia hii hutumika viwandani kuchanganya chakula kwa ajili ya kuku
wanaofugwa katika mashamba makubwa.
Ø Kuchanganya chakula majumbani
(home made ration): Hii ni njia inayotumika
kuchanganya chakula kwa ajili ya kulisha kundi dogo la kuku na njia ambayo
inaweza kutumiwa na wafugaji wadogowadogo.
VIFAA; Beleshi /koleo(spade), Turubai/sakafu safi, Viinilishe , Viroba/Magunia
kwa ajili ya kuhifadhia chakula kilichochanganywa.
Chakula
kilichochanganywa kinaweza kuwekwa katika uzani wa kilo 25-kilo 50, au kilo
100.
Aina ya chakula kiasi
i.
Vyakula vya kutia nguvu mwilini:
Ø Pumba za
mahindi kilo
48
Ø Pumba laini za mpunga kilo 26
Jumla kilo
74
ii. Vyakula cha kujenga
mwili :
Mashudu ya alizeti kilo 18
Damu ya wanyama kilo 1
Mabaki ya samaki
/dagaa kilo
3
Jumla kilo 22
iii.Vyakula vya kuimarisha mifupa (Madini):
- chumvi ya jikoni kilo ½
- chokaa(dicalciumphosphate)… kilo 2
- poultry premix/ kilo ½
- unga wa mifupa kilo 1
Jumla kilo
4
Ø Mahitaji halisi ya viinilishe kwa muhtasari:
Ø Vyakula kutia nguvu mwilini kilo
74
Ø Vyakula vya kujenga mwili kilo
22
Ø Vyakula vya kuimarisha mifupa (Madini) kilo 4
JUMLA 100
Jumla ya mchanganyiko wa vyakula kilo
100
HATUA ZA KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU:
HATUA YA KWANZA:
Katika hatua ya kwanza utaanza kuchanganya vyakula
vya madini
Changanya
, chokaa, chumvi na majivu ya mifupa pig mix vizuri - huu utauita mchanganyo
Na.1
HATUA YA PILI:
Changanya
mchanganyo huo na damu pamoja na samaki waliosagwa - huu utauita mchanganyo Na.
2
HATUA YA TATU:
Mchanganyo
Na.2 uchanganye na mashudu vizuri ambao utauita mchanganyo Na.3.
HATUA YA NNE:
Mchanganyo
Na.3 umwage juu ya rundo la pumba iliyochanganywa (pumba ya mahindi na pumba
laini ya mpunga).
o
Chukua beleshi /koleo safi lililo kavu
na kulitumia kuchanganya rundo la chakula ili kusambaza viinilishe vizuri.
Mambo ya kuzingatia katika
kulisha na kutunza chakula cha kuku:
a) Baada
ya kuchanganya chakula kitawekwa kwenye viroba au magunia na kutunzwa ghalani
(stoo) hadi pale kitakapohitajika kwa ajili ya kulisha kuku.
b) Hakikisha
kuku wanapata lishe kadri inavyopendekezwa na wataalamu.
c) Chakula kilichochanganywa ni lazima kiwekwe
sehemu kavu ili kisiharibiwe na unyevunyevu kama vile kwenye chaga mabanzi
yaliyotandazwa juu ya mawe yalipangwa vizuri
d) Chakula kilichoharibika hakifai kulisha kuku
kwani kinaweza kusababisha matatizo ya afya.
d) Chakula
kilichochanganywa kinatakiwa kisikae muda mrefu baada ya kutayarishwa.
Vyakula vya ziada:
Ili
kuhakikisha kwamba kuku wanapata viinilishe vya kutosha kuku wanaweza kupewa
mchwa na mafunza.
Vilevile
vitu mbadala aina ya nafaka vinavyopatikana hutegemea sana aina ya mazao
yanayolimwa katika eneo husika.
Mbinu za kuotesha mchwa na funza: Funza na mchwa ni chakula kizuri na rahisi chenye viinilishe aina ya
protini kwa kuku wanaofugwa kwa mfumo huria unaoboreshwa. Hata hivyo vyanzo
hivi vya chakula cha protini huchangia tu vile ambavyo kuku wanatakiwa kupewa.
a. Inashauriwa uwape vifaranga hao funza na mchwa kwa sababu ndio
wanaohitaji protini kwa kiasi kikubwa na cha kuaminika.
Funza na mabuu yanaweza kuoteshwa kwa njia rahisi na kutumika kuboresha
chakula cha vifaranga.
c) Mafunza na mabuu yanaweza kuoteshwa kwa kutumia damu, viungo vya
ndani ya tumbo la ng’ombe pamoja na samadi ya ng’ombe.
d) Chungu
kijazwe maji theluthi moja ya ujazo wake, inzi watakuja na kutaga mayai katika
mchanganyiko ambao mafunza walioteshwa wataanza kula mchanganyiko huo.
e) Baada ya
hapo vitu hivi vyote vitachanganywa pamoja katika chungu kimoja kikubwa ambacho
kitaachwa wazi wakati wa mchana na kufunikwa wakati wa usiku.
f) Siku tano
baadaye maji yatajazwa kwenye mtungi huo na mafunza yatakusanywa wakiwa
wanaelea juu. Baada ya kukusanya waoshe vizuri na maji halafu lisha kuku moja
kwa moja.
g) Kumbuka
kuweka chungu kinachooteshwa mafunza kuweka mbali na maeneo ya watu ili kuepuka
harufu inayoweza kusumbua watu.
Makadirio ya chakula cha
kuwalisha vifaranga 100/siku moja:
Umri (wiki baada ya kuzaliwa)
|
Idadi ya
vifaranga
|
Kiasi
kinachotakiwa
Kwa
siku moja(kilo)
|
1
|
100
|
1
|
2
|
100
|
1
|
3
|
100
|
2
|
4
|
100
|
3
|
5
|
100
|
4
|
6
|
100
|
5
|
Maelezo kwa ufupi kuhusu kulisha
kuku:
§ Ni vigumu kukadiria mahitaji ya chakula cha kuku wanaojitafutia chakula,
lakini inakadiriwa kuwa kuku mmoja mkubwa wa uzito wa kilo 1-2 anahitaji
chakula chenye uzani wa gramu 80-160 kwa siku kwa kuku wanofugwa ndani lakini
wale kuku wanafugwa kwa mfumo wa huria nusu huria mahitaji yanakadiriwa
kupungua hadi kufikia gramu 30-50 kwa siku .
§ Ifahamike pia
kuwa kiasi cha chakula hutegemea mahitaji kutokana na uzito na uzalishaji,
mfano kuku anayetaga na anayekua wanahitaji chakula kingi zaidi ya wale ambao
hawatagi au wamekoma kukua.
§ Hakikisha kuku
wanawekewa chakula na maji safi kwenye vyombo safi na kubadilisha kila
vitakapoisha.
ushauri zaidi Wasiliana nasi @kukuproject
Whatsapp (0715-908307 ,0653-691138) au tupigie kwa 07169-457675,0678226498
ushauri zaidi Wasiliana nasi @kukuproject
Whatsapp (0715-908307 ,0653-691138) au tupigie kwa 07169-457675,0678226498