Ujenzi wa mabanda bora ya kuku ni miongoni mwa mambo ya
msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe ni wa asili au wale
walioboreshwa. Hata hivyo si kila mtindo wa ujenzi unafaa, kwahiyo ujenzi huo
ni lazima uzingatie mahitaji halisi ili ufugaji huo uweze kutoa matokeo bora
yanayotarajiwa na mfugaji.
Mambo muhimu katika ujenzi wa banda la kuku ni;
1. Liingize hewa
safi wakati wote.
2. Liwe kavu
daima.
3. Liwe nafasi ya
kutosha.
4. Liwe la
gharama nafuu lakini la kudumu.
5. Lizuie kuingia
wanyama na wadudu hatari kwa kuku.
6. Liwe na nafasi
ya kuweka vyombo vya chakula na maji.
7. Lizuie upepo
wakati wa baridi kali.
HEWA NA MWANGA:
Hewa ni muhimu kwa kila
kiumbe, hivyo banda la kuku ni lazima liingize hewa safi na kutoa ile chafu na
liweze kuingiza mwanga wa kutosha.
1. Kwa kifupi ni
kwamba madirisha ya banda ni lazima yawe makubwa na ya kutosha ili yaingize
hewa safi na kutoa ile chafu.
2. Ni vema
madirisha haya yawe juu kiasi cha meta moja (1) kutoka chini ili hewa ipite juu
ya vichwa vya kuku.
3. Hewa safi siyo
upepo, hivyo jaribu kuzuia upepo mkali kuingia ndani ya banda la kuku ama sivyo
kuku wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa baridi.
4. Jenga Banda lako kwa kukinga upepo unakotokea na
kupanda miti kuzunguka banda hilo la kuku ili kupunguza kasi ya upepo na kuweka
kivuli dhidi ya jua kali na joto.
UKAVU NA USAFI WA NDANI:
Kwa vile kuku si ndege wa majini kama bata , ni jambo la
busara kuhakikisha kuwa mahali anapoishi hapana unyevunyevu.
§ Banda la kuku
lijengwe mahali palipoinuka ili kuzuia maji ya mvua yasiingie.
§ Wajengee kuku
uchaga wa kulalia kwa kuweka viguzo vyenye urefu wa meta moja na kutandika miti
juu yake ili usiku walale hapo, kuliko kuwalaza ardhini au sakafuni.
§ Ukavu wa banda ni
muhimu sana hasa kwa vifaranga na kuku wanaotaga. Ndani ya banda lenye unyevu
mayai kuchafuka sana hata wakati mwingine huoza kwa urahisi na jitihada zako
zitakuwa ni bure.
§ Sakafu ya banda ni
vizuri ikawa ya zege lakini kutokana na uhaba wa fedha sakafu inaweza
kutengenezwa kwa mabanzi (mabanda yaliyoinuliwa) au udongo mgumu na au mchanga
ambao utafunikwa kwa mabaki ya taka za mpunga na yale ya mbao.
§ Ili kuepuka
unyevunyevu ni vyema eneo/mahali pla kujenga banda pawe pameinuka na penye
kupitisha hewa ya kutosha.
PAA LA BANDA:
Paa la banda liwe madhubuti ili kuzuia maji ya mvua kuingia
hasa wakati wa masika. Sakafu ya banda iwe juu zaidi ya usawa wa nje. Paa
linaweza kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati , madebe na kama ikishindikana
tumia nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba katika eneo hilo.
NAFASI YA KUFANYA KAZI:
Banda la kuku lisiwe na nguzo au mbao nyingi sana ndani
kiasi cha kumfanya mhudumiaji wa kuku ashindwe kufanya kazi zake. Hali hiyo
itamfanya apoteze muda mwingi katika kuzizunguka nguzo hizo, hasa wakati wa
kuokota mayai au kufanya usafi.
VIFAA:
Unapotaka kujenga banda la kuku kwanza kabisa tayarisha
vifaa vinavyotakiwa. Vitu kama miti au nyasi, nyavu au fito, misumari au kamba
ni muhimu kuviandaa mapema.
Pili ni lazima uwe na plani/ramani kamili ya banda hilo. Kwa
wastani kila kuku anahitaji nafasi ya Meta za eneo la 0.11 hadi 0.22 (futi 1
hadi 2 za eneo.) kutegemeana na umri wa kuku.
UJENZI RAHISI:
Kuku wafugwao hatimaye ni lazima wafidie gharama za Ujenzi
wa mabanda na chakula. Gharama zikiwa kubwa sana huenda ukaifanya shughuli ya
ufugaji isiwe na faida hata kidogo hali hiyo itamfanya mfugaji aone ufugaji
hauna maana yoyote kwake. Lakini ukijenga banda lako kwa kutumia vifaa
vinavyopatikana kwa urahisi utaongeza faida zaidi kwakuwa umepunguza gharama za
uendeshaji wa mradi.
VIPIMO:
Banda la kuku linatakiwa liwe na Meta 15 hadi
meta 22 za eneo yaani Meta 3 hadi 4.5 za upana kwa meta 5 za urefu. Banda hili
linaweza kutunza kuku 100 wakubwa kwa wakati mmoja.
HITIMISHO;
· Ujenzi wa
mabanda unasisitizwa katika kuboresha ufugaji wa kuku wa asili ili;
· Kuongeza
uzalishaji na kupunguza vifo vya vifaranga kwa majanga mbalimbali kama vicheche
,mwewe, mapaka, mbwa na wizi wa kuku wanaozurura holela.
·
Vile vile inatarajiwa kwamba kuku wanaozuiliwa kwenye banda na kuwekewa
chakula mchanganyiko wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa,Kwa ushauri
zaidiWasiliana nasi @kukuproject au
tupigie,0715908307/0653691138/0678-226498.
1 comment:
Banda kama hilo kwenye picha linaweza kupatikana kwa bei gani? Na linakaa chini au juu ya kitu?
Post a Comment