MAGONJWA YA KUKU:
1) Ugonjwa wa
Mdondo:
Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na unapoingia
kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi kufikia asilimia tisini.
Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwasababu ya usugu mwilini
(body immunity) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi.
. Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha kirusi kiitwacho
Paramyxo viridae na huenezwa kwa njia ya hewa na kugusana.
Dalili zake:
§ Kukohoa na kuhema
kwa shida
§ Ute hutoka mdomoni
na puani
§ Kuku walioathirika
hupata kizunguzungu.
§ Kuharisha uharo wa
kijani na njano
§ Kuzubaa, kusinzia
na mabawa kushuka
§ Baada ya siku 2
kuku hupindisha shingo
§ Kuvimba macho
§ Kuzunguka
§ Kuku hutaga mayai
hafifu.
§ 90% ya kuku huweza
kufa
Tiba:
Ugonjwa huu hauna dawa.
Kinga:
§ Kuchanja;
Chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu /na mara nne kwa
mwaka.
Kuna chanjo aina mbili za ugonjwa huu, nazo ni;
1. Lasota :
Chanjo hii hutolewa katika dawa yenye umbile la kidonge
kimoja kimoja ambacho kina dozi ya kuku 1000 na huwekwa kwenye maji ili kuku
wanywe hiyo dawa.
Inashauriwa kuku wanaopewa dawa hii wanyimwe maji ya kunywa
siku moja kabla yake
Ni vizuri kuwapa
mchanganyiko maalum wa dawa wenye mchanganyiko wa vitamin na dawa ya kuwaongezea kuku nguvu.
Dawa hii itolewe saa moja au zaidi baada
ya kuwapa chanjo ya mdondo.
Thermostable I2 NCD vaccine :
o Huwekwa katika
chupa kimoja (vial) chenye dozi 400 za kuku
o Chanjo hii
inavumilia joto ikikaa bils nje ya jokofu kwa muda mrefu zaidi.
o Imetengenezwa
katika mazingira ya nchi za joto.
Na inaweza kukaa kwa siku 14-15 ikiwa itatunzwa ipasavyo
hata baada ya kutumia mara ya kwanza..
2) Kuharisha Damu
(Coccidiosis):
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha protozoa cha jamii
ya Eimeria (Eimeria tenela, Eimeria maxima, na Eimeria acervulina)
Kwa kawaida wadudu hawa hupenda kuishi kwenye mazingira
machafu, kama vinyesi, vyakula vilivyooza na umaji maji.(moist environments).
Dalili zake:
Kinyesi chake huchanganyika na damu
1) Wakati
mwingine kuku hunya damu.
2) Kuku
hudhoofika sana.
3) Kuku
huteremsha mabawa yake.
4) Hatimaye vifo
hutokea.
Tiba;
Ugonjwa huu hutibika kwa kutumia dawa za
(i) Kundi la suphur
Mfano: sulphonamides (ESB3) kwa siku 3-4
(ii) Amprolium
Dawa za ugonjwa huu hupatikana madukani hivyo ukipatwa na
tatizo hilo fika kwenye maduka ya dawa aua muone mganga wa mifugo.
Kinga:
§ Zingatia usafi mara
kwa mara
Kwakuwa ugonjwa huu huambatana na majimaji na uchafu wenye
vimelea vya ugonjwa huu , ni vizuri
kuhakikisha banda la kuku linakuwa safi na kavu wakati wote.
· Tenga kuku
wagonjwa kutoka kwa walio wazima.
· Tumia dawa ya kinga ili kuepusha uwezekano
wa kuku kuambukizwa ugonjwa huu
Dawa inayopendekezwa ni zile zinzoitwa (coccidiostat.
· Tenga kuku
wadogo (vifaranga) kutoka kwenye kundi la wakubwa.
3) Homa ya
Matumbo(fowl typhoid):
Husababishwa na vimelea vya wadudu wa bakteria wa jamii ya
Salmonella.
Kimelea hicho cha bacteria huitwa Salmonella gallinarum.
Dalili zake:
§ Uharo mweupe au wa
kijani
§ Vifo hufikia kiasi
cha 50%
§ Rangi ya minofu
hugeuka kuwa ya njano
§ Viungo vya ndani
kama maini , figo , bandama huvimba
§ Maini hung’aa
kwenye mwanga mkali.
Tiba :
Tumia dawa za antibiotiki kama vile furazolidone ili kutibu
ugonjwa huu.
KINGA: Chanja kuku wako mara kwa mara .
§ Fanya usafi wa
banda na vyombo vya kulishia na kunyweshea maji ipasavyo.
4) Ugonjwa wa
Mafua ya Ndege:
§ Ugonjwa wa mafua ya
ndege ni ugonjwa hatari sana kwa kuku na jamii nyingine za ndege.
§ Pia ugonjwa huweza
kuambukizwa na kusababisha vifo kwa binadamu.
§ Ugonjwa huu
husababishwa na kirusi kiitwacho Orthomyxo virus.
§ Ugonjwa huu
huenezwa kwa njia ya kugusana baina ya ndege na ndege na baina ya ndege na binadamu.
Dalili zake:
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana katika kipindi cha
siku 3-7 baada ya kuku kuambukizwa.
Dalili hutofautiana kutokana na umri wa ndege.
Baadhi ya dalili zake nihizi zifuatazo
§ Kuku /ndege hupumua
kwa shida (dyspnoea).
§ Kuzubaa.
§ Kutokwa na machozi.
§ Kukohoa na kupiga
chafya.
§ Kuharisha kinyesi
chenye majimaji.
§ Sehemu za kichwa
zisizo na manyoya huvimba.uvimbe wenye majimaji huonekana kichwani na shingoni.
§ Sehemu ya juu
kichwani hubadilika na kuwa na rangi ya bluu iliyopauka.
§ Kuku hutaga mayai
yenye maganda laini.
Tiba:
Ugonjwa huu hauna tiba .
Kinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu:
§ Toa taarifa kwa
mganga (daktari wa mifugo aliye karibu ukiona dalili za ugonjwa huu.
§ Tenga mabanda ya
kuku wagonjwa na walio wazima.
§ Fungia kuku wako
wasitembee holela.
§ Acha kununua kuku
kutoka eneo linalohisiwa kuwa na ugonjwa huu.
§ Acha kusafirisha
mifugo /ndege bila idhini ya daktari.
§ Zuia wageni
kutembelea mabanda yako ya kuku.
§ Acha kuhamisha
mbolea ya kuku kwenda shambani kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa
huu.
§ Safisha mabanda na
kuweka dawa chini ya usimamizi wa mtaalamu wa mifugo na kulipumzisha kwa siku
21kabla ya kuanza kufuga tena.
§ Choma moto mkali au
fukia chini mbolea kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa huu.
§ Pata ushauri kutoka
kwa mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe.
5) Gumboro
(infectious Bursal Disease):
Ugonjwa huu
husababishwa na kirusi
Dalili zake:
o Hushambulia
vifaranga
o Uharo mweupe
o Kuchafuka (dirting
of anal area)
o Kuvimba
o Kiwango kikubwa
cha vifo
o Damu hutapakaa
eneo la kutolea kinyesi
Kinga:
1) Usafi
2) lishe bora
3) chanja
vifaranga wakiwa na umri wa wiki tatu
kwa kutumia chanjo hai (live vaccine)
6) Kifua Kikuu
cha Ndege(Avian Tuberculosis-TB):
Husababishwa na kimelea aitwaye Mycobacterium avium.
DALILI ZAKE:
o Kukonda na
Kupungua uzito
o Vidonda kwenye kishungi
o Kupungua
uzito/kukonda
o Kuhara
Kinga:
Usafi:
Fanya usafi na vyombo , banda na mazingira .
7) Magonjwa
yatokanayo na Lishe (Nutritional and Metabolic Disorders):
Dalili za magonjwa haya hutegemea aina ya virutubisho
vinavyokosekana mwilini
Kwa mfano:
o Kupinda miguu
(rickets) husababishwa na upungufu wa Vit.D, madini ya calcium na fosforasi.
o Vidonda vyenye
vyenye damu husababishwa na vit.K
o Kichaa cha kuku na
kusinyaa kwa misuli husababishwa na upungufu wa Vit.E
o Magamba ya Mayai
(egg shell)kuwa laini ama umbo kuwa bovu husababishwa na upungufu wa madini ya
calcium na fosforasi.
o Kudonoana
kusababishwa kwa njia moja au nyingine na upungufu wa chakula na madini ya
fosforasi na calcium
o Kuvimba macho,
upungufu wa damu huletwa na upungufu wa vit.A.
Kinga:
o Kuwapa kuku mlo
kamili
o Kuelewa kwa kina
aina za chakula kwa kila rika na aina ya kuku ; vifaranga , kuku wa mayai na wa
nyama. (Poultry age and classes i.e chicks, layers and broilers)
o Kufanya uchunguzi
wa virutubisho vilivyomo katika aina ya chakula unachotumia.
8) Minyoo
(Helminthiasis):
Minyoo iko ya aina tatu kama vile minyoo kamba, minyoo bapa
na minyoo ya mviringo
Dalili zake:
§ Kudumaa
§ Kuwa manyoya hafifu
§ Kupungua uzito
§ Kukonda
§ Minyoo huonekana
kwenye kinyesi
KINGA /KUZUIA:
USAFI:
§ Fanya usafi wa
vyombo, banda na mazingira.
§ Tenga vifaranga
kutoka kwa wale wakubwa.
§ Badilisha matandazo
kuondoa mazalia ya minyoo.
§ Badilisha matandazo
kila baada ya miezi mitatu.
TIBA:
§ Tumia dawa
zinazopendekezwa na wataalamu hasa zile zinazoua minyoo ya aina zote (mfano:
piperazine citrate).
§ Hakikisha kila
baada ya miezi mitatu unawapa kuku wako dawa za minyoo.
9) Kupe, Utitiri,
Chawa na Viroboto
kupe laini waitwao
Argus persicus, chawa na viroboto
wanaong’ata .
Dalili zake:
§ Kujikung’uta.
§ Kupiga kelele.
§ Kiasi cha damu
hupungua mwilini.
§ Utando wa ngozi
ndani ya kope za macho hupauka.
§ Utando wa ngozi ya
juu mwilini huwa mnene.
§ Magamba ya
unga-unga hudondoka.
Kuzuia:
§ Tupa au choma
masalia ya mayai yasiyoanguliwa na magamba ya mayai yaliyoanguliwa vifaranga.
Safisha banda mara kwa mara na kunyunyizia dawa; kuna dawa
zinazopendekezwa na wataalamu za kunyunyizia kwenye banda la kuku.
Kwa msaada na ushauri Wasiliana nasi @kukuproject kupitia namba hizi 0715908307/0653691138/0678-226498
No comments:
Post a Comment