Thursday 14 July 2016

UFUGAJI NI SULUHISHO KWA TATIZO LA AJIRA


Kwa miaka mingi nchini Tanzania, na katika baadhi ya nchi nyingine za mashariki mwa Afrika, shughuli za kilimo na ufugaji zimekuwa zikichuku- liwa kuwa ni shughuli za wazee na watu wasio kuwa na uwezo hasa waishio viji- jini, huku vijana wakikimbilia kazi za kuajiriwa maofisini na kwenye biashara mijini.  Kutokana na hali hii uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara ulishuka kwa kiasi kikubwa sana, na kusababisha bei ya vyakula na mazao ya mifugo kuwa ya bei kubwa kutokana na uhaba.   Hali hii pia ilisababisha kuyumba kwa uchumi katika maeneo husika. Watu wenye kipato pia wakitumia fedha nyingi kununulia chakula na mazao ya mifugo na maskini wakiendelea kuwa na maisha duni, na afya hafifu kwa kutoweza kumudu kupata lishe kamili kama inavyotakiwa.  Kwa kuwa sekta hii ni muhimu na inategemewa na kila mtu ingawa haiku- pewa kipaumbele, hali ya uchumi mijini pia ilibadilika na kusababisha vijana walio wengi ambao walikuwa waki- kimbilia humo kujipatia ajira kukosa fursa hiyo.  Na hapa ndipo ule usemi usemao shida ni mwalimu mzuri ulipo- chukua nafasi yake. Hivi sasa, wimbi la vijana wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji, limekuwa likiongezeka siku hadi siku.  Hii inatokana na ukweli kwamba kilimo na ufugaji ndiyo sekta pekee ambayo ina ajira ya uhakika, na uweze- kano wa kujipatia fedha kwa mwaka mzima ni mkubwa mno.  Tumeshuhudia na kusikia kwa siku za karibuni, vijana wanavyohangaika kupata fursa za kujipenyeza kwenye kilimo, na kuweza kufanya shughuli hii kibiashara.   Tunawapongeza wale wote ambao wameweza kugundua kuwa kilimo na ufugaji ni kazi ya heshima na yenye tija kubwa kwa maisha yao. Pia tunawatia shime wale wote ambao bado hawa- jaanza wafanye hivyo, kumbuka, jembe halimtupi mkulima.
  
Kwa wale wote wanaopenda kupata ushauri juu ya ufugaji kuku wasiliana nasi @kukuproject au tupigie  0715908307/0653691138/0678-226498

No comments: