Monday, 11 July 2016

VIDOKEZO MUHIMU JUU YA ULISHAJI WA KUKU



Kuku anayetaga kwa siku huhitaji kiasi cha gramu 130 za chakula pamoja na maji safi wakati wote.


• Kuku mmoja anahitaji wastani wa kilo 2.2 za chakula kwa wiki 8. Hivyo, kuku 100 = 2.2Kg x 100 = 220Kg. Ni lazima kuku waachwe wale muda wote pamoja na kuwapatia maji safi na ya kutosha wakati wote. Wanapomaliza resheni ya chakula cha siku hiyo, wape majani na matunda.


• Mtetea ni lazima alishwe kiasi cha 4.5 Kg za chakula kwa kipindi cha miezi miwili na nusu mpaka aanze kutaga. Baada ya hapo anaweza kuwa kwenye mfumo wa resheni ya chakula kwa kuku wanaotaga. Wapatie pia chakula mbadala kama vile aina ya majani na matunda wanayoweza kula kwenye chakula cha kila siku.


• Mahitaji yote ya chakula kinachotumika ni lazima yawe na kiwango cha juu cha ubora na kinachokubalika. Kamwe usiwape kuku mahindi yaliyooza. Kuku ni rahisi kudhuriwa na sumu aina ya aflatoxin inayopatikana kwenye mahindi yaliyo oza.


• Unapotumia dagaa kuchanganya kwenye chakula cha kuku, hakikisha kuwa hazina mchanga wala makaka ya wadudu wa baharini. Endapo utatumia mahindi hakikisha kuwa yamekauka.


• Chakula cha kuku ni lazima kichan ganywe vizuri ili kuhakikisha uwiano mzuri wa virutubisho.Inashauriwa kutumia pipa kuchanganyia chakula kuliko kutumia beleshi.


• Zingatia kuwa hata baada ya kuwapa kuku chakula chenye mchanganyiko maalumu, ni lazima wapatiwe eneo la wazi wanapoweza kuchakura kwa ajili ya kupata virutubisho vingine kutokana na wadudu ambavyo havikupatikana kwenye chakula.

KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI Tupigie 0715908307/0653691138/0678-226498
AU TEMBELEA PAGE YETU YA FACEBOOK

No comments: